Mchungaji Aliyefufua Mtu Kanisani, Mapya yazidi Kuibuka....



Baada ya kusambaa kwa habari za Mchungaji wa Afrika Kusini Alph Lukau kumfufua mtu katika ibada yake ya Jumapili ya Februari 24, kampuni inayouza masanduku ya mazishi (jeneza) imejitokeza na kusema kuwa sanduku hilo halikutoka kwao, na pia wanafikiria kumshtaki mchungaji huyo.


Akizungumza na Television ya SABC nchini Afrika Kusini, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mazishi ya Kings and Queens, Mis. Vivian Mponda, amesema kwamba wao walifuatwa na mmoja wa wanafamilia wakiomba kutumia usafiri, lakini sanduku lililotumika halikuwa la kwao na wala mwili huo haukuhifadhiwa hapo kama wanavyodai, kwani huwa hawahifadhi mwili bila taarifa rasmi.

“Hatukuwauzia sanduku hivyo sio la kutoka Kings & Queens na hatuna sanduku la vile kwenye mochwari yetu, ila gari walikodi kwetu wakisema wanataka kulitumia kwenye mazishi ya ndugu yao”, amesema Ms. Vivian.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji (SABC) habari zinasema kwamba waandishi walimfuatilia mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Eliot na mpenzi wake ambaye alikuwepo siku ya tukio (kufufuliwa), na kugundua kuwa waliondoka nyumbani kwao tangu Jumatano, na hawajarudi mpaka sasa.

Wakiendelea kuchunguza hilo imebainika kuwa hata mtu aliyesema amempangisha nyumba yake ambaye ndiye alimfia mikononi sio kweli, kwani mwenye yeye ni mwanamke na aliyekuwepo siku ya tukio hilo alikuwa ni mwanaume.


Jumapili ya Februari 24 mchumgaji Alph Lukau wa kanisa la Aleluia Ministry la Afrika Kusini amezua mtafaruku mkubwa mitandaoni baada kudai amemfufua mtu, aliyeletwa na mwenye nyumba wake akidai kuwa alifariki baada ya kumkimbiza hospitali alipoumwa, na ndipo akaamua kumpeleka kanisani kumuombea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad