Mchungaji Atoroka na Kapu la Sadaka Wakati Waumini Wamefumba Macho Kuomba

Mchungaji Atoroka na Kapu la Sadaka Wakati Waumini  Wamefumba Macho Kuomba
Tukio la ajabu limetokea katika kijiji cha Misuu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya baada ya Mchungaji mgeni kutoroka na kapu lililokuwa limejaa sadaka wakati waumini walipokuwa wamefumba macho kuomba.


Kwa mujibu wa moja ya chombo cha habari nchini humo, Mchungaji wa kanisa hilo alimualika mwenzake kutoka kaunti jirani ili awalishe waumini chakula cha kiroho na hatimaye kuongoza harambee ya kupanua kanisa hilo.

“Mtumishi wa Mungu alikuwa na matumaini makubwa kuwa mwenzake angechangisha pesa nyingi katika harambee hiyo kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuongea na kushawishi. Hii ndio sababu kuu ya kumualika kanisani”, amenukuliwa mmoja ya waumini.

Amesema kuwa waumini walipomaliza maombi na kufumbua macho yao, walipigwa na butwaa walipokuta mgeni wao hayupo na kapu la sadaka lilikuwa halionekani.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, juhudi za waumini kumsaka Mchungaji huyo ziliambulia patupu maana alikuwa ametokomea na kila alipopigiwa simu jibu lilikuwa haipatikani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad