Meddie Kagere Mwiba Mchungu Kwa Yanga.....Hakika Hawata Msahau

Baada ya kucheza mchezo wa Club Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa club ya Simba SC na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, Jana ilikuwa ni zamu ya game ya watani wa jadi kukipiga dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa Simba inacheza mchezo huo ikiwa na viporo nane.

Simba ikiwa tena uwanja wa Taifa kupitia kwa yule yule Meddie Kagere imefanikiwa kuifunga Yanga kwa goli 1-0, lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 71, Meddie Kagere anaipatia ushindi Simba kwa mara ya pili mfululizo upande ule ule wwa goli, hiyo ni baada ya kuwalaza Al Ahly mapema wiki iliyoisha.

Ushindi huo sasa umeifanya Simba kufikisha jumla ya point 39 wakiwa wamecheza michezo 16 jumla huku Yanga wao wakiwa  na point 58 wakiwa wamecheza michezo 24, hivyo ni tofauti ya michezo nane dhidi ya Simba, hadi dakika 90 zinamalizika Simba walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 60 kwa 40.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad