Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametilia shaka uwezekano wa klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Premia msimu huu.
Lakini ameongeza kuwa hakuna haja ya kufanyia marekebisho kikosi chake ili kushinda taji hilo.
United wameshinda mechi 9 kati ya 10 tangu Solskjaer alipochukua nafasi ya Jose Mourinho alifutwa kazi mwezi Disemba mwaka jana.
Manchester United wanashikilia nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Premia, wakiwa nyumba ya mahasimu wao Liverpool na Manchester City kwa alama 14.
"Mwaka huu tuko mbali kidigo, bila shaka,"alisema Solskjaer.
Meneja wa Fulham Claudio Ranieri anaamini kaimu meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anastahili kupewa kazi ya kudumu
"Inabidi tukimbizane na timu zilizo mbele yetu, hususan City, Liverpool na Tottenham - pia wamekuimarisha mchezo wao.
"miaka miwili' sio muda mrefu, lakini pia sio muda mfupi wa kusema tunaweza kuonesha tofauti kubwa katika maandalizi yetu, na kila kitu."
Raia huyo wa Norway wa miaka 45 ambaye alishinda Tuzo ya meneja wa mwezi wa ligi ya England mwezi Januari tayari ana ''taswira'' ya jinsi "Hii timu ya Manchester United itakavyo kuwa katika kipinda cha miaka michache", hata kama hatapewakazi ya kudumu.
Alipoulizwa klabu hiyo inahitaji wachezaji wangapi ili kushinda taji hilo, Solskjaer alisema: "inategemea pia utendakazi wa wachezaji waliopo kwa sasa.
Meneja wa Man U: Kikosi Changu Kinahitaji Miaka miwili kushinda EPL
0
February 09, 2019
Tags