Mfahamu Kwa Undani Mnyama Kangaroo, Anatumika Kama Alama ya Taifa


Kangaroo ni wanyama wenye miguu mifupi sana ya mbele, kiasi cha kumfanya hata akimbiapo kutumia miguu miwili ya nyuma huku mkia wake ukimpa msaada mkubwa katika 'balance' ya mwili
-
Madume huwa wakubwa kuliko majike na wanyama hawa hufikia uzito wa kilo mpaka 90 na urefu wa futi 6. Dume hutofautiana na jike kwa muonekano wa rangi ambapo huwa kama wekundu mgongoni na majike huwa wa kijivu
-
Kangaroo ni mnyama mpenda amani na si mkorofi hata kwa mtoto wake, isipokuwa madume tu ndiyo hupenda kupigana hasa wanapopenda sehemu moja
-
Mapigano yao ni ya kustaajabisha kwani miguu ya mbele hutumia kwa kushikana huku wakitumia miguu yao ya nyuma kupigania na kurusha mateke
-
Maadui zao wakubwa ni wawili, Simba pamoja na Tai, ambaye mara kwa mara hufanya majaribio ya kutaka kuiba watoto wa Kangaroo
-
Kangaroo jike ana mfuko ambao hutumia kubebea mtoto wake
-
Kama Tanzania tunavyomuheshimu Twiga ndivyo hivyo hivyo anavyoheshimika Kangaroo nchini Australia. Ni alama ya utambulisho wa Taifa hilo na amewekwa katika ngao ya Taifa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad