Mkazi wa kitongoji cha Ukindo kijiji cha Lugalawa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe aliyefahamika kwa jina la Osmund Joseph Mwinuka anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 amefariki dunia kwa kuchomwa na kisu maeneo ya tumboni na mke wake kwa sababu ya Mapenzi.
Akizungumza na mtandaao huu kwa Njia ya simu mmoja wa mashuhuda aliyefika katika tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake,amesema kuwa mwanaume huyo fundi piki piki na mkulima wa kijiji hicho alichomwa na kisu na mke wake Marselina Mtweve majira ya jioni baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea kilabuni.
“Kwa kweli wananchi walikuwa na hasira kali ila huyu mama alichukuliwa na askari jana ilele maana wananchi walitaka kumpiga na usiku ule ule Yule mwanaume alipochomwa na kisu alipelekwa hospital akafia njiani
"Ila usiku alipokamatwa ilipofika asubuhi watoto wakubwa wawili walichukuliwa na kwenda kutolea ushahidi mtoto mmoja alieleza kuwa baba na mama walikuwa wanagombana ndipo mama akachukua kisu akamchoma baba akaenda kukiosha baada ya hapo akaenda kuficha ardhini ndipo akaunyanyua mlango ukae vibaya ili watu waseme alijingonga mlangoni ndipo akaenda kupiga kelele majirani waje yaani huyu mama alikuwa akijichanganya kwa kila mtu”alisema mwananchi
Aliongeza kuwa wananchi wa kijiji hicho wanasikitishwa na kitendo hicho kwani mama huyo amekuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yake na kusababisha kumkwaza mume wake mara kwa mara lakini mama huyo ameamua kuchukua uamuzi huo ili kuepusha usumbufu aliokuwa akiupata kutoka kwa mume wake.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu.Erasto John Mhagama amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo katika eneo lake huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa ni mgogoro wa Mapenzi.
“Chanzo cha yote hayo ni wivu wa mapenzi kwasababu nilikuwa naongea na yule mama wakati mgonjwa amefikishwa hospital, akasema chanzo cha mgogoro wetu ulianzia kirabuni mpaka tumefika nyumbani ndipo alipomchoma na kisu kwasababu alimwambia anatembea na wanaume wakati sio kweli na hawa nininavyofahamu mimi wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara”alisema mwenyekiti
Hata hivyo mtandao huu ulimtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Renata Mzinga ambaye amethibitisha kuzipokea taarifa hizo.
“Ni kweli taarifa hizo zipo,ila kwa sasa tunamaliza kwanza hili la watoto nitatoa taarifa”alisema Kamanda Mzinga
Mtuhumiwa huyo mwenye watoto saba kwa marehemu amefikishwa katika kituo cha polisi wilayani Ludewa huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.
Mke Amuua Mumewe Kwa Kumchoma Kisu Tumboni Wilayani Ludewa
0
February 16, 2019
Tags