Mo Dewji aweka wazi adhabu watakayopewa wachezaji

Mo Dewji aweka wazi adhabu watakayopewa wachezaji
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema bado timu hiyo ina nafasi ya kushinda mechi zake za kundi D kwenye Ligi ya Mabingwa na kuingia hatua ya robo fainali.

Akiongea leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimio ya kikao cha Bodi ya wakurugenzi kilichofanyika Jumatano wiki hii, Mo amesema moja ya mambo yaliyojadiliwa ni nidhamu na kujituma kwa wachezaji.

''Kuna uwezekano wapo wachezaji wasio na nidhamu na hawajitumi kwenye klabu, niseme tu kwamba hao mikataba yao ikiisha hatutaendelea nao labda wabadilike'', amesema Mo.

Mbali na hilo Mo Dewji amesema ndoto yake, bodi pamoja na wanasimba kwa ujumla ni kutwaa ubingwa Afrika ndani ya miaka mitano ijayo hivyo kinachofanyika hivi sasa ni uwekezaji ili timu iweze kushindana vizuri.

Kwa upande mwingine Mwekezaji huyo anayemilika asilimia 49 ya hisa za klabu ameweka wazi kuwa kwasasa timu inatafuta kocha msaidizi na pia hivi karibuni zitatangazwa nafasi za kazi ili kupata wataalamu katika kila idara kwaajili ya kufanikisha uendeshaji wa kisasa wa klabu.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad