Monalisa: Sina Bifu na Kajala Ila Naona Watu Ndiyo Wanataka Kutugombanisha

Monalisa: Sina Bifu na Kajala Ila Naona Watu Ndiyo Wanataka Kutugombanisha
KUTOKANA na yaliyotokea hivi karibuni kuhusu watoto wao na tetesi kuzagaa kuwa wameingia kwenye bifu, msanii wa filamu za Kibongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amefunguka kuwa hana bifu na Kajala Masanja ila watu ndiyo wanataka kuwagombanisha.



Akistorisha na Risasi Jumamosi, Monalisa alisema watu wamekuwa wakizungumza maneno mengi ambayo yanaweza kusababisha wagombane wakati wao wako vizuri, hawana tofauti yoyote kama watu wanavyosema.

“Sina bifu na Kajala ila naona watu ndiyo wanataka kutugombanisha, naomba watu waache maneno jamani ili maisha mengine yaendelee maana kila siku ni hilohilo tu,” alisema Monalisa.



Mtoto wa Kajala, Paula na mtoto wa Monalisa walikuwa wakisoma shule moja ambapo walihitimu kidato cha nne hivi karibuni huku mtoto wa Monalisa aitwaye Sonia akifanya vizuri na Paula akifanya vibaya hivyo kusababisha maneno yaliyoonekana kuwagombanisha wazazi; Monalisa na Kajala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad