Msimamo wa Serikali juu ya Mashamba ya Mo Dewji



Serikali imesema mashamba sita  yanayomilikiwa na Mohamed Dewji ambaye ni mfanyabiashara maarufu yapo chini ya uangalizi na iwapo atashindwa kutekeleza masharti watayafuta.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Lukuvi amesema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo katika mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki.

Aidha amesema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita bado sita ambayo yapo kwenye uangalizi na kubainisha kuwa Tanzania ina mashamba makubwa 2000 ya kilimo na ufugaji.

Lukuvi amesema kwa kipindi cha miaka mitatu wamefuta mashamba 46 katika maeneo mbalimbali ambayo yameshindwa kutimiza masharti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad