Mti Wenye Miaka 400 Waibiwa Japana
0
February 15, 2019
Wanandoa wawili wanaomiliki mti aina ya Bonsai wameanzisha kampeni iliojawa na hisia kwa wezi walioiba miti saba kutoka kwao , huku wakitoa ombi la kuwaangalia 'watoto'' mti huo.
Seiji Iimura na mkewe Fuyumi wanasema kuwa miti hiyo yenye bei ghali iliibiwa kutoka kwa bustani yao huko Saitama karibu na Tokyo.
''Hakuna maneno ya kuelezea tunavyohisi'', bwana Iimura aliandika. Ilikuwa miti yenye thamani kubwa kwetu''.
Miti hiyo midogo ina thamani ya $118,000, kulingana na ripoti ya CNN.
Ikidaiwa kutoka mashariki mwa Asia na kuhusishwa na Japan, Bonsai ni aina ya sanaa kutokana na mbinu za kilimo cha kitaalamu.
Miti hiyo midogo hupandwa katika mikebe. Uhitaji kuangaliwa kwa utaalamu wa kiwango cha juu na hufanana na miti mikubwa iliostawi.
Mojawapo ya miti ilioibiwa ni ule wa Shimpaku Juniper-mojawapo ya miti inayotafutwa sana baada ya ile ya Bonsai.
Unadaiwa kuwa na thamani ya zaidi ya $91,000.
''Mti wa Shimpaku uliishi kwa takriban miaka 400, unahitaji uangalizi na hauwezi kuishi kwa wiki bila kunyunyuziwa maji'', bi Imura aliambia CNN.
''Unaweza kuishi milele hata baada ya sisi tumeondoka. Nataka mtu yeyote yule aliyeuchukua kuhakikisha kuwa unatiwa maji vizuri'', Alithibitisha kwa BBC siku ya Jumanne kwamba bado miti hiyo haijapatikana.
"Tuna huzuni lakini tutaendelea kuilindia miti yetu ya Bonsai Bi limura aliandika katika mtandao wa facebook. Kwa sasa Tutaendelea kupanda miti inayopendwa na kupongezwa na watu wote'',
Wakulima wa Bustani na wapenzi wa miti ya Bonsai walituma jumbe kwa familia za Imura mtandaoni kuonyesha huruma na ushirikiano
'Hawasameheki ujumbe mmoja ulisema katika chapisho: '' hawa wezi hawajui maana ya kuiba mti mmoja wa wa Bonsai wa misaba''.
Miti ya Bonsai inafaa kuheshimiwa na lazima iwe zaidi ya tamaa za kibinadamu. Nimevunjika moyo kusoma hili'', mtu mwerngine aliandika