Muungano mpya upinzani wapewa rungu kuanza kazi

Muungano mpya upinzani wapewa rungu kuanza kazi
Vyama vya upinzani nchini vimeazimia rasmi kuanza kutekeleza azimio la Zanzibar baada ya taratibu za mawasiliano ndani ya muungano huo kukamilika.

Hayo yamezungumzwa na Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kuwa vyama vyote vilivyosaini azimio hilo juu ya kuungana katika masuala mbalimbali, vimekubaliana kuanza utekelezaji wake.


Vyama hivyo viliazimia kwa pamoja Desemba 19 mwaka 2018 kuungana katika masuala mbalimbali katika vikao vilivyofanyika visiwani Zanzibar. Vyama vilivyosaini azimio hilo ni CHADEMA, CUF, ACT wazalendo, Chauma, NLD na NCCR-Mageuzi.

Moja ya makubaliano ambayo yalifikiwa katika azimiom hilo ni suala la kudai demokrasia nchini, bila kujali juu ya katazo la serikali la kutofanya shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad