Mwanaharakati Aliyekatwa Kenya Akutwa Mochwari

Mwanaharakati Aliyekatwa Kenya Akutwa Mochwari
POLISI nchini Kenya wamesema kuwa uchunguzi wa awali uanaonyesha kuwa kifo cha mwanaharakati maarufu, Caroline Mwatha, kimetokana na kutoa ujauzito wa miezi mitano.



Mara ya mwisho kwa mawanaharakati huyo kuonekana hai ilikuwa Jumatano ya wiki iliyopita kabla ya mwili wake kugunduliwa kwenye chumba cha kuhifadia maiti cha City Mortuary mjini Nairobi.



Mwatha ni mwanaharakati aliyefanya kazi katika shirika la haki la kijamii katika kitongoji cha Dandora mjini Nairobi, shirika linalonakili visa vya mauaji ya kiholela yaliyotekelezwa na maofisa wa polisi hususan katika vitongoji vinavyoshuhudia uhalifu mkubwa jijini Nairobi.



Kumekuwa na hofu kuwa kifo hicho kimetokana na kazi zake ambazo jamii inaziona ni hatarishi kwa usalama na maisha.



Lakini taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoti, inasema kuwa makachero wanaamini mwanaharakati huyo alifariki wakati alipokuwa akitoa ujauzito Jumatano ya wiki iliyopita, (Februari, 6), siku ambayo alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai.



Inasemekana kuwa Mwatha ni mke na mama wa watoto wawili.    Ni mkasa uliozusha mjadala miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii.









Kampeni za kutaka kujua ukweli wa aliko bi Mwatha, ambaye kwa takriban wiki moja leo, alikuwa hajulikani aliko, zilianzishwa katika mitandao ya kijamii.



Makundi ya kutetea haki za binaadamu likiwemo Amnesty International na hata mengine kama Missing Voices, yalishinikiza kutafutwa kwa Mwatha waliyemtaja kama “mtetezi wa dhati wa haki za binadamu”.



Kwa siku kadhaa familia na marafiki wa marehemu inasemekana wamekuwa wakizunguka katika hospitali mbalimbali na hata vyumba vya kuhifadhia maiti wakimtafuta mwanaharakati huyo.






Kwa mujibu wa vyombo vya habari chini Kenya, Mwatha amekuwa akifuatilia mauaji yanayofanywa kiholela na polisi nchini Kenya.



Kuna habari zinazosema, mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti na mtu binafsi, na haijulikani wazi ni lini hasa alipopelekwa.



Kwa sasa, polisi inajaribu kuchambua ni wapi na vipi alivyofariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad