MWANAMKE mfanyakazi katika gereza kutoka Missouri, Marekani anatuhumiwa kuwa alimuua mumewe kwa kumtilia sumu kwenye chakula, ili waoane na mpenzi wake mfungwa. Amy Murray, wa miaka 40 alishtakiwa Ijumaa kwa mauaji ya mumewe Joshua Murray wa miaka 37, ambaye alipatikana akiwa maiti mnamo Desemba 11.
Japo mwanamume huyo alipatikana kitandani akiwa maiti, ripoti ya upasuaji wa mwili wake ilionyesha kuwa alikufa kutokana na kutiliwa sumu, kabla ya mtoto kuwashwa ndani ya nyumba yake. Ni hapo ambapo wachunguzi katika kesi hiyo walibaini kuwa Amy alikuwa akifanya kazi ya uuguzi katika jela ya Jefferson na alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfungwa Eugene Claypool, wa miaka 40.
Amy anasemekana kuanzisha moto huo kisha akaondoka nyumbani kwake na mwanawe mvulana na mbwa wawili. Lakini mshukiwa alieleza wachunguzi kuwa aliporejea nyumbani alipata nyumba ikiwaka moto na moshi ulikuwa mkubwa hivi kwamba hangeweza kuingia.
Lakini wachunguzi walipata rekodi ya mawasiliano baina ya Amy na mpenzi wake mfungwa, ambapo alikuwa akimwambia kuwa hakutaka tena kuwa katika uhusiano wa ndoa na mumewe. Katika mawasiliano mengine, alimwambia Claypool kuwa angemuoa kwa kuwa mumewe sasa alikuwa amefariki na hangezuia kitu.
Wawili hao aidha walizungumzia kuhusu kumtafutia mfungwa huyo wakili ili aachiliwe mapema. Claypool alikamatwa mnamo 2000 na amekuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 18, kwa kosa la kumdunga kisu mwanamume wa miaka 72 ambaye alishinda zaidi ya Sh100milioni katika mchezo wa Kamari. Amy na mumewe Joshua walikuwa wameoana tangu 2003 na walikuwa na mtoto wa kiume.
Mwanamke Amuua Mumewe kwa Kumpa sumu ili Afunge Ndoa na Mchepuko
0
February 16, 2019
Tags