Mwijage Aeleza Alivyoonekana Dodoma hadi Chato Baada Kutoka Mbio Bungeni Baada ya King'ora cha Hatari

Mwijage aeleza alivyoonekana Dodoma hadi Chato
Baada ya kuzua mjadala kupitia mitandao ya kijamii Waziri wa zamani Viwanda na Biashara Charles Mwijage amefunguka sababu ya yeye kukimbia Bungeni wakati ilipotokea sauti iliyoashiria kuwa ni ya hatari.

Juzi wakati tukio hilo likitokea, wabunge wote walilazimika kutoka nje lakini mjadala mkubwa ulikuwa kwa Mbunge huyo wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage ambapo wengi walimtafsiri kuwa ni muoga.

Mwijage amesema, "nilikuwa na wenzangu wakati alarm inalia nikawaambia wenzangu tulieni, nilivyoona mlango wa kuingilia Spika unafunguka kwa kiasi kikubwa kwa hiyo niliondoka haraka iwezekanavyo ili ule mlango usifunge."

"Kuhusu mimi kuwa muoga ulikuwa ni mzaha tu kwasababu kuna mwenzangu alikutana na mtu Dumila akajua ni mimi, mwingine aliniona Kibaigwa, wengine walioniona Chato lakini kiuhalisia huwezi kufika maeneo yote hayo kwa masaa mawili."

Juzi February 5, 2019 Bunge lililazimika kuahirishwa kwa muda mara baada ya kutokea taharuki kufuatia alarm ya tahadhari kulia wakati kikao kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad