Mzee Akilimali amesema hayo licha ya Yanga kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 58 ambazo ni 22 mbele ya Simba wanaoshika nafasi ya nne.
Mzee Akilimali ameliambia Championi Jumatano, kuwa wapinzani wenzao Simba wanaweza kutwaa ubingwa kutokana na vitu ambavyo Yanga wanafanyiwa ikiwemo kunyimwa mabao ya halali.
“Imeshapangwa Simba itwae ubingwa mwaka huu, sisi tumekuwa tukinyimwa mabao ya wazi mfano kule Tanga.
“Haya matokeo tunayoyapata ni kutokana na juhudi za wachezaji tu na si vinginevyo, hivyo mimi na wazee wenzangu wote tunakubaliana na lolote litakalotokea ni sawa,” alimaliza Mzee Akilimali. Wakati huohuo, Akilimali amesema hata mchezo wa Jumamosi ambao Simba watavaana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam anaamini kuwa Simba watashinda.
“Sioni dalili za kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo, sioni kabisa nakwambia kwa sababu Simba wanapendwa na TFF ndiyo wanawabeba.
“Angalia wao wana kila kitu, sisi timu inajiendesha kwa michango hadi kocha anatoa pesa yake mfukoni kuwalipa wachezaji ulipata kuona wapi, naona wazi wanatafunga watakavyo nakwambia,” alisema Mzee Akilimali