Nabii Shepherd Bushiri Anayepaa Angani Akamatwa
0
February 03, 2019
Nabii mwenye utata raia wa Afrika Kusini Shepherd Bushiri wa kanisa la Enlightened Christian Gathering Church (ECG) ametiwa nguvuni.
Bushiri alikamatwa Ijumaa, Februari 1, jijini Rustenberg, Afrika Kusinia na kulingana na taarifa kutoka kanisa lake nabii huyo na mke wake wanatuhumiwa kwa ulanguzi wa pesa.
Raia kadhaa Afrika Kusini walijitokeza mtandaoni na kusimulia walivyolaghaiwa pesa na Bushiri.
Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, kukamatwa kwa nabii huyo kunajiri saa chache baada ya kuondolewa lawama kuhusu kisa cha waumini kukanyagana katika kanisa lake.
Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu 3. "Ukikumbuka kutokea mwaka jana tumesumbuka na tuhuma eti baba yetu alihusika na mganyagano uliotokea.
Amekamatwa na anahojiwa na makachero jijini Silverton, Pretoria," taarifa kutoka kanisa hilo ilisema.
Msemaji wa Bushiri kwa jina Maynard Manyowa alisema polisi walifika alfajiri na kumchukua nabii na mke wake na walidai walitaka kusema nao.
“Baadaye tuligundua ni wanachama wa Hawks. Walimchukua nabii watu na mama Mary Bushiri, waliwafunga pingu na kuwapeleka Pretoria," taarifa hiyo ilisema.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, mamia ya watu wamekuwa wakilalamika kupitia mtandao kuhusu Bushiri kulaghaiwa pesa.
Reneilwe Mphahlele alidai kuwa, alipeana R21 000 (158,310.96 KES) wakati wa Pasaka 2017 ili kuonana ana kwa ana na mchungaji huyo.
Kulingana naye, anajutia kwa sababu hamna mabadiliko yoyote aliyoyaona baada ya kumwona Bushiri na kwamba sasa anafahamu Mungu ni wa kila mtu na hatolewi pesa.
Haijabainika wazi ikiwa ufichuzi wa punde kutoka kwa watu unahusiana kivyovyote na mashtaka yanayomkabili Bushiri.
Nabii Bushiri si mgeni katika kuhusishwa na kashfa zenye utata lakini inashangaza jinsi anavyoendelea kuwa na ufuasi mkubwa wa watu katika kanisa lake la ECG.
Karibuni alichapisha video mtandaoni akidai kuwa na uwezo wa kupaa angani wakati akihubiri.
Tags