Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amegawa vitambulisho 40,000 katika Halmashauri nane za Mkoa huo ambapo amesikitishwa na kasi ya utoaji wa vitambulisho kwa Wafanyabiashara wadogo zoezi ambalo katika awamu ya kwanza limefikia asilimia 28, ametoa maagizo mapya.
“Mkurugenzi atakayeshindwa kukusanya fedha inayotakana na malipo ya vitambulisho hatufai, tutamuondoa, Mkuu wa Wilaya anajua hatari inayomkabili, Mkuu wa Mkoa ninajua hatari inayonikabili," alisema RC Mwanri.
"Maneno yaliyokuwa yanapita wakati Mkuu alikuwa anazungumza nilikuwa sina hakika kama ajira hii ipo au imeondoka ,nani atakubali niondolewe kwenye Ukuu wa Mkoa nikachukue lile jembe la Kisukuma si watanifukia. Mimi hapa kabla Mkuu hajaniondoa nafyeka wote hapa Faap! nasema nileteeni wengine," RC Mwanri aliongeza.