Nape ataja sababu kujiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii

Nape ataja sababu kujiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema, amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ili apate muda wa kufanya kazi jimboni kwake. Amesema yanayozungumzwa kuhusu uamuzi wake ni mambo ya barabarani hivyo yaachwe huko.

Nape amesema kuwa amechukua uamuzi huo kwa kuwa umebaki muda mfupi kwa yeye kutimiza alichowaahidi wananchi jimboni kwake na kwamba anataka aache alama kwenye jimbo hilo hivyo akiendelea na kazi nyingine atashindwa.

Kauli hiyo ameitoa jana Februari 6,2019, na kuongezea kuwa CCM inapaswa kutafuta majibu kwa kizazi cha vijana badala ya kuendelea kutegemea historia kama mtaji wa kuendelea kubaki madarakani kwani isipofanya hivyo inaweza kupata shida kwa kuwa vijana ni kundi kubwa na hawaijui historia.

"CCM ikiweza kutafsiri ukuaji uchumi kutoka kwenye karatasi kwenda kwenye maisha ya wananchi itawavutia vijana wengi watakaopiga kura mwaka 2020 kwa kuwa itaboresha huduma za msingi zikiwemo za maji, afya, barabara, elimu na nyinginezo", Amesema Nape.

Ameongeza kuwa CCM ipo madarakani kwa sababu wananchi wanakipenda chama hicho, hivyo lazima kifanye mambo yatakayosababisha kiendelee kupendwa na kisifanye mambo ikaonekana inapindapinda, inatumia nguvu, na inapaswa kushawishi mioyo ya watu kupitia kazi zake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad