NIDA: Usajili na Utambuzi wa Wanchi ni Bure
1
February 21, 2019
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa Huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa ajili ya kupatiwa Kitam- bulisho cha Taifa inatolewa BURE. Mwananchi anatakiwa kufika katika ofisi za NIDA akiwa na nakala (Photocopies) za viambatisho vyake muhimu.
Waombaji wote wa Vitambulisho vya Taifa mnakumbushwa kuwa “Rushwa ni Adui wa Haki. Usikubali kudai, kutoa wala kupokea Rushwa.” Kitambulisho cha Taifa ni haki yako ya msingi na hakiuzwi.
Hakikisha unahudumiwa katika Ofisi au Vituo rasmi vya Usajili vya NIDA na Afisa wa NIDA na sio Vishoka wanaojipenyeza kwenye zoezi.
Ukiombwa Rushwa Toa Taarifa kwa Mawasiliano :-
Simu: 0800758888 au 0673 333 444 au 0759102010 au 0765201020, Barua: S.L.P 12324 Dar es Salaam, Barua pepe (email): nida.tanzania@nida.go.tz. Tembelea tovuti yetu: www.nida.go.tz, Facebook nidatanzania, twitter @nidaTanzania au twitter.com/nidatanzania
Imetolewa na:- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Tags
Hongereni sana NIDA.
ReplyDeleteHuku ndio Kutuelimisha na Mawasiliano yenu Mmetupa Wazi Kabisa/
Huu ndio utandawazi na Uzalendo ambao tunautegemea.
VITAMBULISHO NI HAKI YETU/
NAOMBA MUWEKE MABANGO BARABARANI NA KWENYE OFISI ZA NIDA ZISEMAZO.
"NDUGU MWANANCHI KITAMBULISHO NI HAKI YAKO"
"TUPO HAPA KUKUHUDUMIA MPAKA UMEKIPATA WEWE NA FAMILIA YAKO"
HAKINA MALIPO ZAIDI YA UTAMBULISHO WAKO KISHERIA.
KARIBU KATIKA KULIJENGA TAIFA .. NA TANZANIA YETU MPYA..!!!