Ninja kushuka dimbani dhidi ya Simba SC kesho

Ninja kushuka dimbani dhidi ya Simba SC kesho
Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuwa mchezaji na beki wake, Abdallah Shaibu 'Ninja' atahusika katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga kupitia Radio Magic FM, Dismas Ten, amesema Ninja atacheza kama endapo Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera atampendekeza na akikanusha kupewa adhabu yoyote na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Awali kulizuka taarifa kuwa TFF kupitia Bodi ya Ligi wamemfungia Ninja michezo mitatu kwa kitendo cha kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Coastal Union katika mechi ambayo ilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya mabao 1-1 huko Mkwakwani, Tanga.

"Hakuna barua rasmi inayoeleza kuwa Ninja amepewa adhabu ya kifungo cha mechi 3, hivyo Ninja mpaka sasa atahusika katika mechi ijayo dhidi ya Simba endapo Mwalimu ataamua atumike" alisema.

Yanga itakuwa mwenyeji Februari 16 Jumamosi ya wiki hii katika dimba la Taifa ambapo itakuwa inawaalika watani zao wa jadi Simba kusaka alama tatu muhimu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad