Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumia watawa kama watumwa wa ngono

Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumia watawa kama watumwa wa ngono
Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumikisha kingono watawa wa kanisa hilo na kwamba tatizo hilo limekuwa likiendelea

Alisema kuwa mtangulizi wake Papa Benedict, alilazimika kufunga shirika la zima la watawa ambao walikuwa wakidhulumiwa kingono na makasisi.

Inaaminiwa kuwa hii ni mara ya kwanza Papa Francis amekiri hadharani kuhusu dhulima za kingono dhidi ya watawa wa kanisa hilo kubwa zaidi duniani.

Papa Francis apokea barua ya rais Nicolas Maduro
Kwanini ziara ya Papa huko Arabuni ni muhimu ?
Amesema kuwa kanisa limejaribu kukabiliana na tatizo hilo na kwamba juhudi hizo bado ''zinaendelea''.

Papa alitoa tamko hilo kwa wanahabari akiwa kwenye ziara yake kihistoria katika eneo la mashariki ya kati.

Alikiri kuwa makasisi na maaskofu wamekuwa wakiwanyanyasa watawa, na kwamba kanisa "linashughulikia suala hilo".

"Ni mpango ambao tumekuwa tukiendeleza,"alisema.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwezi Novemba mwaka jana kongamano la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki duniani lililaani "utamaduni wa ukimya na usiri" ambao unawazuia kuzungumzia changamoto wanazopitia.

Papa Francis awatahadharisha watawa kuhusu matumizi ya mitandao
Siku chache zilizopita jarida la wanawake wa Vatican linalofahamika kama Women Church World lililaani vikali unyanyasaji huo ikiongeza kuwa katika visa vingine watawa wanalazimishwa kuavya mimba ya makasisi hao kwasababu kuwa na watoto-ni kitu kinachoenda tofauti na maadili ya ukatoliki.

Jarida hilo limesema vugu vugu la #MeToo limewasaidia wanawake wengi kujitokeza na kusimulia visa vyao

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad