Polisi Kenya Yadai Mwanaharakati Amekufa Wakati Akitoa Mimba

Polisi Kenya Yadai Mwanaharakati Amekufa Wakati Akitoa Mimba
Polisi nchini Kenya wamesema kuwa uchunguzi wa awali uanaonesha kuwa kifo cha mwanaharakati maarufu Caroline Mwatha kimetokana na kutoa ujauzito wa miezi mitano.

Mara ya mwisho kwa mawanaharakati huyo kuonekana hai ilikuwa Jumatano ya wiki iliyopita kabla ya mwili wake kugunduliwa kwenye chumba cha kuhifadia maiti cha City Mortuary mjini Nairobi.

Caroline Mwatha ni mwanaharakati aliyefanya kazi katika shirika la haki la kijamii katika kitongoji cha Dandora mjini Nairobi, shirika linalonakili visa vya mauaji ya kiholela yaliotekelezwa na maafisa wa polisi hususan katika vitongoji vinavyoshuhudia uhalifu mkubwa Nairobi.

Washukiwa wa mauaji ya watoto Tanzania wapandishwa mahakamani
Muhandisi maarufu wa Tanzania ashinda tuzo Marekani
Wizi wa mti ulio na miaka 400 wazua majonzi Japan
Kumekuwa na hofu kuwa kifo hicho kimetokana na kazi zake ambazo jamii inaziona ni hatarishi kwa usalama na maisha.

Lakini taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai George Kinoti inasema kuwa makachero wanaamini mwanaharakati huyo alifariki wakati alipokuwa akitoa ujauzito Jumatano ya wiki iliyopita, (Februari, 6), siku ambayo alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai.

Caroline inaarifiwa ni mke na mama wa watoto wawili.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya wapelelezi, kuwa marehemu alikuwa kwenye mazungumzo ya simu ya mara kwa mara na mwanaume mwengine ambaye si mumewe kuhusu ujauzito huo. Plisi wanadai alikuwa ni mpenzi wake.

Mwanaume huyo, wapelelezi wanadai ndiye aliyefanya mazungumzo na kituo cha kutolea mimba kilichopo eneo la Dandora Phase I, Nairobi na kutoa kima cha Sh6,000 ili kazi hiyo ifanyike.

Baada ya kufikwa na umauti, polisi wanasema mwili wa Croline ulipelekwa Nairobi City Mortuary saa 10 usiku ya Februari 7.

Watu sita, ikiwemo bwana huyo aliyekuwa akiwasiliana na marehemu, mmiliki wa kituo cha afya inachodaiwa alifariki ndani yake na dereva wa gari ya kukodi (Uber) wanashikiliwa na polisi mpaka sasa huku uchunguzi zaidi wa mkasa huo ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad