Polisi nchini Uganda imewazuia waandishi habari wa BBC katika mji mkuu, Kampala, Waandishi hao walikuwa wakifuatilia taarifa kuhusu uuzaji haramu wa dawa za Serikali na walikamatwa Jumatano usiku.
Msemaji wa Serikali ya Uganda Ofwono Opondo ametaka waachiliwe mara moja, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters na kusema kuwa bado hajafahamu ni kwa misingi gani polisi iliwakamata waandishi habari hao, kwa mtazamo wake walikuwa wanaisaidia serikali kufichua muozo ulioko kwenye mfumo wanapaswa kuachiliwa pasi masharti.
Katika taarifa ya BBC imesema imewasiliana na maafisa husika na inashughulika kuitatua hali iliopo.