Polisi Wakamata 28 kwa Tuhuma za Mauaji Watoto Njombe


Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kupitia Kamanda wa Mkoa Renata Mzinga limesema linawashikilia watu 28 wakiwemo wafanyabiashara kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watoto ambayo yameonekana kushika kasi hivi karibuni.

Utakumbuka siku ya Jumamosi mtoto wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili aliuawa kikatili na kutelekezwa kichakani Lupembe mkoani  Njombe wakati akitoka shuleni.


Mkoa wa Njombe umekuwa ukikabiliwa na matukio ya watoto kutekwa na kuawa kikatili kwa siku za hivi karibuni.

Wiki iliyopita Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 walipatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad