Rais Karia amtaja Tundu Lissu mkutano mkuu TFF


Katika mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Rais Wallace Karia amewaonya wale wote wanaojifanya ni kina Lissu wa mpira na kuweka wazi kuwa hatacheka nao.


Karia ameeleza kwa manufaa ya mpira wa Tanzania ni lazima viongozi wawe na nidhamu na kuheshimu kanuni na miongozo ya mpira duniani vinginevyo ataendelea kuwafungia.

“Siwezi kuwachekea wanaojifanya akina Lissu kwenye mpira wetu, nitaendelea kuwafungia ili mpira wetu uwe salama'', amesema Karia katika hotuba yake.

Mbali na hilo Karia ameeleza mipango mbalimbali ya shirikisho hilo katika kuinua mchezo wa soka ikiwemo kuanzisha ligi mbalimbali za vijana.

Uongozi wa Karia ulichanguliwa mwaka 2017 katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Dodoma ambapo Karia alichaguliwa kuwa Rais huku makamu akiwa ni Michael Wambura lakini ameshafungiwa maisha kujihusisha na soka.


KARIA AOMBA MSAMAHA

Rais wa TFF Wallace Karia amekiomba msamaha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutokana na kumtolea mfano mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu.

Karia amesema alimfananisha Lissu na Wambura kwasababu wote wanakwenda kwenye vyombo vya habari kusema mabaya kwa viongozi waliochanguliwa kiuhalali kabisa.

''Sikumaanisha vibaya lakini kama kuna watu hilo limewakwanza basi naomba msamaha lakini siku maanisha vibaya'', - Karia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad