Rais Kenyata wataka wauguzi waligoma kurudi kazini

Rais Kenyata wataka wauguzi waligoma kurudi kazini
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata amewataka wauguzi wanaoshiriki mgomo kusitisha mgomo na kuripoti kazini ifikapo Ijumaa, February 15 mwaka huu saa mbili asubuhi.

Hapo juzi mgomo wa madaktari na wauguzi nchini Kenya umeingia juma la pili, huku maelfu ya wagonjwa wanao tafuta huduma katika hospitali za umma wakikosa kupata matibabu.

Majimbo kumi kati ya 47 ya nchini Kenya tayari yanashiriki mgomo huo huku mengine 19 likiwemo jimbo la Nairobi palipo na jiji kuu la nchi hiyo wakitoa taarifa ya kuanza mgomo huo iwapo mazungumzo yanayo endelea yatagonga mwamba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad