Rais Magufuli Aitembelea Familia ya Kigwangala Kuwafariji na Msiba

Rais Magufuli Aitembelea Familia ya Kigwangala Kuwafariji na Msiba
Rais Dkt. John Magufuli, leo ametoa mkono wa pole kwa familia ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye amefiwa na mwanae aitwaye Zul Hamis Kigwangalla jana Februari 21, 2019 Jijini Dar es Salaam.



Rais Magufuli akiwa na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wamefika nyumbani kwa familia hiyo maeneo ya Vitoria, Mikocheni A, jijini Dar es Salaam na kuwapa pole baadhi ya wanafamilia wakiwamo Mama wa Marehemu, Dkt. Bayoum Kigwangalla waliokiwa katika maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Nzega Mkoani Tabora kwa mazishi.


Aidha, baba wa marehemu, Dkt. Hamis Kigwangalla tayari ameshatangulia Nzega ambako mazishi yatafanyika baadaye leo jioni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad