Rais Magufuli atoa neno kijana aliyepigwa risasi


Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amefika nyumbani kwa kijana Richard Peter, ambaye amefariki siku za hivi karibuni kwa kupigwa risasi akiwa katika kituo cha polisi.

Akizungumza mbele ya familia hiyo ambapo alifika kwa ajili ya kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Magufuli, Lugola amesema polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.

Lugola amesema “alipopata taarifa zilimshtua na sababu moja kubwa ya kumshtua ni kwamba amefia kwenye eneo la polisi, kwa hiyo amenituma niwapeni pole sana”

"Niwaombe watanzania mliamini jeshi la polisi maana si jehi la kuua watu na wala hatufundishi askari wetu kuua watu kwa hiyo isitafsiriwe jeshi letu ni la kuua watu muwe nasubira" ameongeza Kangi Lugola.

Waziri huyo kwa sasa yuko ziarani Mkoa wa Arusha ambapo siku ya kwanza alizungumzia kuhusiana na tukio la kushambuliwa na Tundu Lissu pamoja na kuzungumza na madereva wa bodaboda mapema jana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad