Rais Magufuli Atoa Wito kwa vyombo vyote vya TV na Redio


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vyote vya Tv na Redio kuhakikisha wana wajibu wa kutoa mambo chanya katika nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipotembelea kituo cha Channel Ten ambapo sambamba hilo amewataka wafanyakazi wa ofisi hizo kuchapa kazi.

"Natoa wito kwa vyombo vyote vya Tv na Redio mna wajibu wa kutoa yaliyo positive katika nchi yetu lakini pia muendelee kutoa elimu , Tanzania asilimia 75 ni wakulima vipindi vya kuonyesha uvugaji bora, ukulima bora hivi navyo ni muhimu kwa Watanzania kuviangalia," amesema Rais Magufuli.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad