Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua gari la Mahakama inayotembea litakaloweza kuisaidia usikilizwaji wa mashauri katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam.
Rais John Magufuli, Jaji Mkuu Ibrahim Juma,
Uzinduzi wa gari hilo la kisasa lenye umeme ndani yake, umefanyika leo Februari 6, 2019 katika maadhimisho ya siku ya sheria.
Gari hilo hadi kukamilika kwake limegharimu TSh Milioni 470.82 huku likiwa na TV, kamera zenye uwezo wa kurekodi ushahidi wote kwa picha na sauti, lifti kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza ratiba ya mahakama hiyo.
Gari hilo limeelekezwa kuanza kufanya katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza, hii ni kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya watu na shughuli za kiuchumi.
“Hatuna mahakama nyingi za kutoa huduma katika maeneo hayo, mfano katika eneo la Nyamagana tuna mahakama mbili za mwanzo zinazohudumia kata 18, Ilemela mahakama mbili kata 19 na Dar es Salaam wakazi wa Chanika wanalazimika kufuata huduma Ukonga,”.
Rais Magufuli azindua ‘mahakama inayotembea’, wananchi kesi zao kusikilizwa mtaani
0
February 06, 2019
Tags