Rais Mstaafu Mkapa atangaza kujiuzulu

Rais Mstaafu Mkapa atangaza kujiuzulu
Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa amefikia maamuzi ya kujiuzulu nafasi yake kiongozi wa jopo la usuluhishi wa mgogoro wa Burundi baada ya kuteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa (RFI)  Benjamini Mkapa amefikia maamuzi hayo baada ya kudai jumuiya hiyo kushindwa kuunga mkono jitihada za kumaliza mgogoro huo.

Januari 31, Benjamin Mkapa aliwasilisha baadhi ya ripoti kwenye jumuiya hiyo ambayo mpaka sasa haijawekwa wazi nini ambacho kilielezwa kwenye ripoti hiyo.

Kuhusiana na mgogoro huo Benjamin Mkapa amesema "serikali na upinzani wanapaswa kuzungumza na kukubaliana kuhusu mfumo wa kisheria na taratibu zinazohitajika kufanyika kwa uchaguzi ujao.

Aidha Mkapa ametoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo yatakayo washirikisha wadau wote kwa kufuata iliyowekwa katika mazungumzo ya awali na ameomba viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushiriki.

Katika mkutano wa 17 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha 2016 uliamzimia kumteua Rais huyo Mstaafu wa awamu ya tatu kuwa kiongozi wa jopo la usuluhishi wa mgogoro wa kiungozi nchini Burundi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad