Ratiba ya Ligi Kuu Yaibana Mbavu Simba

BAADA ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mechi ya ne ya kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya soka ya Simba itakuwa na ratiba ngumu katika mechi zake zijazo.



Kinachofuata sasa ni kwamba Simba imeanza maandalizi tayari kwa mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya mahasimu wao, Yanga, ambao utapigwa Jumamosi, Februari 16, 2019,  kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kinachofuata ni kusafiri  Jumapili kwenda Arusha ambapo itafanya mazoezi kwa siku moja kabla ya mechi yake dhidi ya African Lyon itakayopigwa tarehe 19.



Itarejea Dar es salaam na kujianda kwa siku moja kisha kushuka dimbani tarehe 22 dhidi ya Azam FC na kesho yake itasafiri kwenda Iringa na itakuwa na siku mbili za mazoezi ambapo itacheza tarehe 26 dhidi ya Lipuli FC.


Baada ya mchezo huo itaunganisha kwenda Shinyanga na itakuwa na siku mbili  tu za mazoezi kabla ya Machi 3 kuivaa Stand United ambapo baadaye itarudi Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda Algeria Machi 6/ kwenda kucheza na JS Saoura Machi 9.



Simba inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama sita nyuma ya Al Ahly yenye alama saba huku JS Saoura wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama tano na AS VItal wakishika mkia wakiwa na alama nne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad