Ray C Afungukia Mipango Yake Ya Kufunga Ndoa na Mzungu Wake


Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na kuanzisha familia na mpenzi wake ambaye anaishi naye nchini Uingereza.

Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi nyingi kuwa mwanadada huyo kwa sasa ana maisha mazuri mno huko London baada ya kuchumbiwa na m[enzi wake ambaye ni mzungu ambaye ana watoto wawili;


Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Ray C ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na kuanzisha familia ughaibuni na pia kuendeleza sanaa yake;

"Mimi nipo na nina kazi (nyimbo) ambazo nilipozitoa zilifanya vizuri sana na zinaendelea kufanya poa sana. Kama watakumbuka mwaka juzi niliachia Wimbo wa Umezima, mwaka jana nikaachia Hatuachani na Rogaroga hivyo si kweli kwamba nipo kimya. Mwaka huu watege sikio maana mambo mazuri yanakuja.

Ni kweli muda mwingi niko nje ya nchi kwenye shughuli zangu binafsi, lakini nikipata shoo huwa ninafanya. Kwa mfano wiki hii nina shoo Houston (Texas, Marekani). Hivyo shoo zipo tu na zikija za huko Bongo wataniona tu.

Ukiona nipo London, ujue nipo kwa fiancee (mchumba) wangu (amechumbiwa na Mzungu, raia wa Uingereza). Ukweli ni kwamba sijaolewa, lakini nina mchumba ambaye tupo kwenye process (taratibu) za kufunga ndoa.

Natamani sana kumzalia mchumba wangu na nina mpango huo, sema acha niolewe kwanza kwani mtoto wa ndoa ana baraka zake"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad