RC Gambo Azidi Kuwasha Moto Sakata la Twiga Kuuliwa


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd imekuwa ikikaidi maagizo ya serikali wilaya ya Longido kulipa madai ya vijiji jambo ambalo halikubaliki.

Kauli hiyo inakuja mara baada ya kuagiza mmiliki wa Kampuni hiyo kuripoti mbele ya kamati aliyoiunda ili kueleza sakata la kuuawa Twiga katika kitalu chake na kushindwa kuvilipa vijiji 23 kiasi cha sh 329 milioni.

Mkuu huyo wa mkoa amezungumza hayo katika wilaya ya Karatu, katika hafla yakabidhi vitambulisho 10,000 kwa wafanyabiashara wadogo.

“Hii kampuni wanamaneno mengi sana nawaambia hivi serikali ya awamu hii haina maneno inasimamia sheria popote walipo wajitokeze katika kamati ili kubaini mambo ambayo tumegundua awali na waache kutisha watu," amesema RC Gambo.

Ameendelea kwa kusema, 'Taarifa zao tunazo na nakwambia DC Mwaisumbe nipo nyuma yako katika hili simamia sheria na kanuni zilizopo hakuna mtu yoyote kukatisha kwa jambo lolote lazima tuchukue hatua,'.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad