RC Makonda atoa Tsh. Milioni 5 kwa mama wa Godzilla


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Tsh. Milioni 5 kwa Mama mzazi wa
Godzilla kama sehemu ya kutimiza malengo ya marehemu aliyokuwa ameyaweka kwa mama yake
kabla ya kukutwa na umauti.

RC Makonda ameeleza hilo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa mpendwa Godzilla inayofanyika katika viwanja vya Salasala Dar es Salaam.

"Ndugu yetu alikuwa na mipango wa kumsaidia mama yake kiuchumi, akawa amempa milioni nne
lakini akawa na malengo ya kumpa milioni tano  ili aweze kuanzisha famasi kama sehemu ya
kujitengemea kiuchumi," amesema.

Amesema kuwa baada ya Godzilla kuanza kuumwa mama yake alitumia fedha hizo, hivyo yeye atatoa Milioni tano ili kumuwesha mama Godzilla.

RC Makonda amesema fedha hiyo itatoa siku ya Jumatano na msanii Fid Q ndio atakabidhiwa ili akamkabidhi mama yake Godzilla.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad