Roma Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa 'Rostam'

Roma Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa 'Rostam'
Mkali wa Hip Hop nchini, Ibrahim Mussa 'Roma' amefunguka juu ya tetesi za kuvunjika kwa kundi la Rostam linaloundwa na yeye mwenyewe pamoja na msanii Stamina

Akizungumza katika Friday Night Live (FNL), Roma amesema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote kwakuwa kazi zao zinaendelea kama kawaida chini ya management yao.

"Makundi mengi huvunjika kwasababu ya mambo mawili, pesa na wanawake, lakini bahati kwenye mabinti, mimi na Stamina tumefanikiwa na kwenye pesa pia tuko sawa. Rostam hatuwezi kuvunjika hata kidogo", amesema.

Pia amezungumzi namna alivyomsimamiwa na Billnass katika uandishi wake wa mashairi ya wimbo huo kwa kuhofia kupeleka ujumbe mzito kwa jamii.

"Mwanzoni aliniongoza vizuri, uzuri alinipa 'content' ya wimbo wote kuwa wimbo uitwe 'Funga gate' akanielewesha kitu gani niwasilishe lakini hakuishia hapo, aliniongoza sana hadi studio alikuwepo akihofia kuwa ninaweza kubadilisha nikaingiza 'leta wajeda'", ameongeza Roma.

Tetesi za kuvunjika kwa kundi la Rostam zilishika kasi baada ya Roma kuachia wimbo wa kolabo na Billnass mwishoni mwa mwezi Januari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad