Msanii wa Bongo Fleva, Rosa Ree ametangaza kuachana na lebo iliyokuwa ikimsimamia kimuziki,
Dimo Prodution kutoka nchini Afrika Kusini.
Rapa huyo ameeleza kutokana na sababu zisizozuilika ndani ya kampuni, kuanzia October mwaka jana hakuwepo chini ya lebo hiyo ambapo aliendelea kufanya kazi na timu yake ya siku zote.
"Kando na hayo napenda kushukuru kwa nafasi niliyoipata ya kufanya kazi na kampuni hiyo na
naamini tumefanya mengi makubwa na yenye manufaa kwetu sote," ameeleza Rosa Ree kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ameeleza kuwa tangu alipoanza kufanya pekee yake ameweza kutoka ngoma mbili ambazo ni Banjuka na Asante Baba.
Rosa Ree alitangazwa kuwa chini ya Dimo Production May 39, 2018, kwa mujibu wa lebo hiyo
mkataba na msanii huyo ulikuwa wa kipindi cha miaka mitatu.
Pia ilielezwa kuwa Rosa Ree amepatiwa nyumba yenye thamani ya Tsh. Milioni 400 Dar es Salaam,
na nyumba nyingine Afrika Kusini.
Wimbo wa kwanza kwa Rosa Ree kutoa chini ya lebo hiyo ni Way Up aliomshirikisha rapa Emtee kutoka Afrika Kusini, wimbo mwingine ni One Way. Dimo Production ni lebo ya pili kwa Rosa Ree kimuziki baada ya kufanya kazi na The Industry.