Washtakiwa hao kwa pamoja walisomewa mashtaka 12 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Wakili Swai alidai mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka hayo 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Washitakiwa hao bado wanasota rumande kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.