Rushwa yaiweka pabaya Afrika kusin

Rushwa yaiweka pabaya Afrika kusin
Serikali ya Afrika kusini imeelezea kusikitishwa kwake baada ya Marekani na balozi nyingine za Ulaya kumuandikia barua Rais Cyril Ramaphosa wakimtaka kuchukua hatua zaidi za kupambana na rushwa na kuimarisha mazingira mazuri ya biashara kwa wawekezaji.

Serikali imesema balozi hizo zimevunja protokali.

Alipoingia madarakani mwaka mmoja uliopita, baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa rais Zuma, Rais Ramaphosa alisema kushughulikia tatizo la rushwa ni jambo litakalokuwa kipaumbele chake kikubwa.

Ukosoaji huo wa serikali yake umekuja miezi michache tu kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo na wakati ambao nchi hiyo inahitaji vitega uchumi vya kigeni.

Taarifa ya serikali imesema Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Afrika kusini atazungumza na na mabalozi wa Marekani na Ulaya ambao wamevunja protokali kwa kuilalamikia moja kwa moja ofisi ya Rais.

Gazeti la Afrika kusini la Sunday Times limesema kuwa barua ya mabalozi hao imemuonya Rais Cyril Ramaphosa kwamba vitega uchumi vya wageni viko hatarini, isipokuwa kama hatua zitachukuliwa dhidi ya wala rushwa na kama kutakuwa na msimamo wa kisiasa katika utawala wa sheria.

Kwa kipindi cha miezi sita tayari aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Rais wa nchi Cyril Ramaphosa anajua kwamba utawala unaweza kuimarishwa na hiyo itasaidia kuvutia wawekezaji wa kigeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad