Sakata la unyanyasaji wa kingono bado lalitikisa kanisa katoliki, Papa Francis aitisha mkutano mzito wa kimataifa

Sakata la unyanyasaji wa kingono bado lalitikisa kanisa katoliki, Papa Francis aitisha mkutano mzito wa kimataifa
Katika jitihada za kukabiliana na shutuma za unyanyasaji wa kingono katika kanisa katoliki, Papa ameitisha mkutano wa aina yake na maaskofu mjini Rome.


Hii inafuatiwa na madai ya baadhi ya mapadre kuwanyanyasa watawa kwa kuwatumikisha kingono katika makazi ya watawa nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Papa Francis aliamua kuitisha mkutano wa kimataifa baada ya kujadiliana na makadinari tisa ambao walichaguliwa mara baada ya Papa Francis alipochaguliwa.

Papa akiwa katika shinikizo kubwa la kutoa uongozi ambao unaweza kutafuta suluhu kwa kile kinacholeta mgogoro katika kanisa kwa sasa.

Simulizi za unyanyasaji zimekuwa zikijitokeza katika kila kona ulimwenguni.Na kanisa limekuwa likishutumiwa kwa kutetea uhalifu wa mapadre.

Papa Francis pia anapaswa kukabiliana na ukweli uliopo, mitazamo na vitendo ambavyo vinapelekea utamaduni wa unyanyasaji kukua.

Aidha kiwango cha changamoto hizi inaweza kuthibitishwa.

Mwandishi Jason Berry ni miogoni mwa watu wa kwanza kuweka wazi unyanyasaji ambao upo katika kanisa
Mkutano huu ambao umehudhuriwa na askofu wakuu katika kila nchi kutoka katika nchi zaidi ya 130, ndio mwanzo mzuri ambao unaashiria kuwa ugonjwa ambao umekuwa ukilisumbua kanisa katoliki tangu mwaka 1980, sumu yake inaweza kutolewa.

Wakati ambapo mwandishi Jason Berry kutoka gazeti moja nchini Marekani alianza kufuatilia mienendo ya padre Gilbert Gauthe, aliyekuwa anashutumiwa kwa unyanyasaji wa kingono.

Kipindi mwandishi huyo alipoandika taarifa ya padre huyo hakutegemea kuwa itasambaa ulimwenguni na hata baada ya miaka 30 kuendelewa kukumbukwa.

Kazi ya Bery ilipelekea kutungwa kwa kitabu kinachoitwa ‘Lead us into temptation’ kilichotolewa mwaka 1992, kilicholenga hatua za kisheria kufuatwa kwa washitakiwa kadhaa mwishoni mwa mwaka 1980.

Majimbo sita kati ya nane ya kanisa katoliki katika mji wa Pennsylvania yalifanyiwa uchunguzi mwaka jana.

Mashaidi kadhaa walitoa ushuuda wao na viongozi wengine wa dini walikubali makosa yao.

“Zaidi ya waathirika 1000 waliobanika walikuwa ni watoto , na shutuma zilikuwa zinawakabili mapadre zaidi ya 300”.

Ripoti yenye kurasa zaidi ya 1,000 ziliangazia unyanyasaji uliofanyika kwa miaka 70 iiyopita.

Downside Abbey
Katika jimbo la Scranton, padre alimbaka msichana ambaye alipopata mimba na padre huyo kumtaka kutoa mimba .Huo ni ushaidi ambao uliandikwa kwaa meneja wa mapadre kwa njia ya barua.

“Huu ni wakati mgumu sana katika maisha yako ambapo unaweza kutambua namna ambavyo umesikitishwa na vitendo vinavyoendelea, hata mimi ninasikitika pamoja nawe.”

Barua ilikuwa imeandikwa kwa padre.

Katika jimbo lingine, padre alimtembelea mtoto wa miaka saba hospitalini na kumbaka.

Tukio lingine lilikuwa la unyanyasaji kwa mtoto wa miaka tisa la kumwagia maji ya baraka.

Padre Franco Mulakkal aliondolewa katika kanisa moja dogo kusini magharibi mwa nchini India na kupelekwa kuwa askofu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Padre huyo alikamatwa mwezi septemba mwaka 2018, baada ya kushutumiwa na watawa kuwa alikuwa anatembelea katika makazi ya watawa na kumbaka sista mmoja kila mara. Askofu huyo ambaye ametolewa katika wadhifa wake kwa muda amekana kuhusika na shutuma hizo dhidi yake.

Catholic nuns in Kerala, who are demanding the arrest of Bishop Franco Mullakal of Jalandhar for allegedly raping a nun multiple times

Watawa wa kanisa Katoliki la Kerala nchini India, wanataka Padre Franco Mulakkal, wa Jalandhar, kukamatwa kwa makosa ya ubakaji
Katika barua iliyoandikwa na masista/watawa wamedai kuwa sista huyo alidai kuanza kubakwa kwa mara ya kwanza ilikuwa mwezi mei mwaka 2014 na mwisho wa askofu huyo kumbaka ilikuwa Septemba mwaka 2016.

Huku nchini Malawi ,zaidi ya asilimia kumi ya masista wana maambukizi ya virusi vya Ukimwi wakati inafahamika kuwa wao hawashiriki ngono.

Jambo hili kutojirudia tena
Mwaka 2012, serikali ya Australia ilitangaza kufanya uchunguzi katika taasisi ili kubaini unyanyasaji dhidi ya watoto.

Taasisi zilizojumuishwa ni pamoja na shule, timu za mpira, sanaa, makundi ya jamii na kanisa.

Asilimia saba ya mapadre wa kanisa kaoliki walishutumiwa na unyanyasaji kwa watoto ndaini ya mwaka 1950 mpaka 2010.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad