Serikali Kuendelea kumuenzi mgunduzi wa Madini ya Tanzanite

Serikali Kuendelea kumuenzi mgunduzi wa Madini ya Tanzanite
Serikali imeahidi itaendelea kumuenzi mgunduzi madini ya Tanzanite, Jumanne Mhero Ngoma (80) aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita.

Akizungumza wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Jumamosi Waziri wa Madini, Dotto Biteko, alisema Serikali inatambua na kuheshimu ugunduzi wa Tanzanite uliofanywa na Mzee Ngoma.

Alisema ugunduzi wake umeijengea Tanzania heshima kubwa Duniani kote na kuboresha maisha ya watu wengi ndani na nje ya nchi kutokana na kazi zake nzuri.Alisema Mzee Ngoma ni shujaa wa Taifa.

"Inasikitisha kuona kuna baadhi ya wenzetu ambao wana tabia ya kuenzi ugunduzi uliofanywa na watu wa nje na kupuuza ule unaofanywa na Watanzania, si ajabu kusikia ya kuwa kuna Watanzania wenzetu ambao pia walipinga ugunduzi uliofanywa na Mzee Ngoma, jambo ambalo halipendezi," alisema na kuongeza;

"Sisi kwa upande wetu kama Serikali tutaendelea kumuenzi Mzee Ngoma na ugunduzi wake alioufanya na wakati huo huo kukabiliana na wale wote ambao wanalenga kudhoofisha na kuhujumu kazi nzuri aliyoifanya shujaa huyu wa Taifa letu, hii ndiyo itakuwa siku zote tofauti yetu na wale wote wasioitakia mema Tanzania na watu wake."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad