Serikali yafunguka Kutochunguza Shambulio la Lissu
1
February 03, 2019
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk. Abdallah Possi ameeleza sababu za kushindwa kuendelea kwa chunguzi wa shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu kuwa ni kutokana na kutopata ushirikiano kutoka kwa mbunge huyo.
Dk. Possi ametoa tamko hilo wakati akijibu madai ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyoyatoa hivi karibuni nchini humo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha News Africa cha kituo cha televisheni cha Deutsche Welle (DW).
Akijibu madai ya Lissu katika tamko lake la Januari 29, 2019, Dk Possi amesema Serikali imekuwa ikilifuatilia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuanza uchunguzi na kwamba amesema mamlaka za Serikali zingetaka kumpata Lissu ili atoe ushirikiano.
“Hadi sasa vyombo vya sheria havijapata ushirikiano wa mbunge huyo na dereva wake ili kupata taarifa muhimu za siku hiyo. Uchunguzi kwa Tanzania bado ni muhimu na bado unawasubiri wao kwa kuwa walishuhudia kwa macho ili waeleze kilichotokea,” ameongeza Dk Possi.
Aidha Balozi Possi amemtaka Mbunge huyo kupima ishara njema za Rais na kwamba kwenye madai anayotoa hayana msingi.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa taarifa ya kulaani tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa kina wa haraka. Kwa nyakati tofauti Rais amemtuma Makamu wake, Rais mstaafu na viongozi wengine wa Serikali kumtembelea Lissu akiwa hospitali akiwa Dodoma, Nairobi na Brussels (Ubelgiji).” Dk. Possi
Naye Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas katika ukurasa wake wa Twitter ameeleza kwamba "bado ubalozi unasubiri miadi ya DW kutoa tarehe kwa mahojiano kufafanua zaidi".
Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu kufuatia shambulio la risasi la Septemba 7, 2017 jijini Dodoma.
Tags
Kichwa Cha Habari hakiendani na maudhui. Si sahihi na NI Cha kichochezi.
ReplyDeleteTafadhalini mkisahihishe.
Mgeweza kutumia Kusitisha kama inabidi.. Ukweli mnajua kuwa suala linaendelea kuchu guzwa na vyombo husika na kwa wakati muafaka