SERIKALI imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya watu wa kada mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, kuwa korosho inanunuliwa chini ya Sh3,300 kinyume na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli.
Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, ametoa ufafanuzi huo bungeni kuhusu bei ya korosho leo Februari 4, 2019 akibainisha kuwa korosho inanunuliwa kwa Sh 3,300 kwa kilo moja, na kwamba maagizo ya Rais hayajakiukwa.
Mgumba amesema kiasi cha Sh 3,300 kinalipwa kwa korosho daraja la kwanza, ambapo daraja la pili hununuliwa kwa Sh 2,640.
Mgumba alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe, aliyetaka kujua kwa nini wanunuzi wa korosho wamekiuka agizo la Rais Magufuli na kuanza kulipa chini ya kiwango ambacho hakikuelekezwa.
Serikali Yatoa Ufafanuzi Jinsi Inavyonunua Korosho Chini ya Bei Elekezi
0
February 04, 2019
Tags