Shilole Achoka Kumpigania Zari kwa Diamond Platnumz


Mara baada ya msanii wa Bongo Fleva, Shilole kumshauri Diamond Platnumz kumuoa aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzie, Zari The Bosslady, sasa inaonekana ameamua kubadili upepo.

Licha ya Diamond kuweka wazi kuwa yupo kwenye mahusiano na Tanasha, Shilole alionekana kutovutiwa kabisa na mapenzi yao.

Ingawa mara kadhaa alisikika akimshauri Diamond kurudiana na Zari, sasa amekubali kishingo upande Diamond aendelee kuwa na Tanasha.

"Anapopenda kaka yangu sina jinsi! Hi Tanasha, Diamond Platnumz wifi yetu karibu Dada hii ndo Tanzania nitafanyaje sasa Jamani," ameeleza Shilole.

Utakumbuka wiki mbili zilizopita Shilole alifanya mahojiano na Wasafi TV na kusema; 'Nitafurahi sana Diamond akioa ila katika kuoa kwake ajaribu kurudisha kumbukumbu nyuma, amuoe Zari hata kama atamuoa mwanamke mwingine sijiu nani anaweza kumfaa,'.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Diamond kuachana na Zari na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo Natasha kutoka nchini Kenya. Hivi karibuni Diamond Platnumz alikaririwa na kituo hicho cha runinga akieleza kuwa ndoa yake aliyopanga kuifunga mwezi wa pili mwaka huu ameisogeza mbele.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad