Mchezo huu ambao Yanga itawakaribisha Simba Uwanja wa Taifa unatarajiwa kubeba hisia za mashabiki kutokana na namna ushindani unavyokuwa kwa timuhizi mbili zinapokutana.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza msimu huu Simba walikuwa wenyeji Uwanja wa Taifa na dakika 90 zilikamilika kwa suluhu ya kutofungana.
Ikumbukwe kuwa nyota wa mchezo alikuwa ni mlinda mlango wa Yanga Beno Kakolanya ambaye leo hatakuwepo kutokana na matatizo yake binafsi na timu.
Pia tukio ambalo lilikuwa gumzo ni mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu kutoa nje mpira wa kwanza dakika ya kwanza.
Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 23 huku Simba wakiwa nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 15 wakiwa nafasi pointi 36.