Simu ya kwanza duniani yenye kamera tano kuzinduliwa mwezi huu

Simu ya kwanza duniani yenye kamera tano kuzinduliwa mwezi huu
Kampuni ya Nokia ipo mbioni kuzindua simu yake mpya ya Nokia 9 Pureview yenye kamera 5 za nyuma zenye ukubwa wa Megapixel 20 na flash.

Kwa mujibu wa mtandao wa GSMArena.com umeeleza kuwa, Nokia 9 Pureview inatarajiwa kuja na kioo cha inchi 5.99 ambacho kitakuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, huku kikiwa na resolution ya 1440 x 2960 pixels.

Mbali na yote Nokia 9 inakuja na teknolojia za kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof) yenye uwezo wa kufanya simu hiyo kukaa kwenye maji yenye kina cha urefu wa mita 1.5 kwa dakika 30.

Nokia 9 Pureview inakuja pia na processor ya Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm), yenye speed ya Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver), pamoja na ukubwa wa ROM au ukubwa wa ndani wa GB 128 vyote vikiwa vinasidiwa na RAM ya GB 6.

Kwa upande wa Betri, Simu hii inatarajiwa kuja na betri yenya ukubwa wa Li-Po 4150 mAh yenye uwezo wa kukaa na chaji kuanzia siku mbili hadi tatu.

Simu hiyo, inatarajiwa kuzinduliwa Februari 12, 2019, kwenye mkutano wa MWC 2019, kampuni nyingine za vifaa vya Kielekroniki vitaonesha bidhaa zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad