Simu ya Mkononi ya Zitto Kabwe Yashikiliwa na Takukuru

Simu ya Mkononi ya Zitto Kabwe Yashikiliwa na Takukuru
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeishikilia simu ya mkononi ya Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tuhuma zake kwa baadhi ya viongozi wa serikali aliyodai wamehongwa ili kukwamisha mradi wa Mchuchuma na Liganga.



Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na mke wa mbunge huyo kupitia Twitter, imesema TAKUKURU imeishikilia simu hiyo kwa ajili ya uchunguzi huku akiwataka ndugu, jamaa na marafiki kutoitumia simu hiyo (kuipigia au kuiandikia ujumbe) kwa sababu kwa sasa haipo mikononi mwa Zitto.


Mwishoni mwa mwaka jana, Zitto alilalamika kupitia mitandao ya kijamii hususan Twitter akisema mradi wa Mchuchuma na Liganga unahujumiwa na makampuni ya chuma kutoka China, Urusi na Uturuki na kudai wapo baadhi ya viongozi wa juu serikalini katika mradi wa uzalishaji chuma wa Mchuchuma na Liganga, ambapo aliitwa TAKUKURU na kupeleka ushahidi wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad