Siwezi Kumuacha Mwanangu Alie Peke yake - Kajala Masanja Afunguka


Muigizaji wa Filamu,  Kajala Masanja, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu matokeo ya mtoto wake, Paula ya kidato cha nne.

Kajala amesema kuwa anashangazwa na inaumiza watu wanaacha kazi na kuanza kumrushia maneneo makali mwanae, amesemaa kuwa hata muacha mwanae aliye peke yake.

"Nashangazwa na inaumiza watu wanaacha kazi na kuanza kumrushia maneno makali mwanangu kwa lengo la kumkatisha tamaa, yaani kama ndio waliokuwa wakimlipia ada na huduma zingine. Watambue kuwa siwezi kumuacha mwanangu alie peke yake, nitakuwa naye kumtia moyo na kujipanga upya katika elemu yake na atasoma hadi chuo kikuu," Kajala ameiambia Mwanaspoti. Kajala.

Matokeo ya Mtoto wake huyo yalizua gumzo kwenye gumzo mtandaoni wiki moja iliyopita, ambapo mpaka sasa Msanii huyo hajaweka wazi matokeo ya mtoto wake huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad