Spika Ndugai: Baada ya Simba Yakupigwa bao 5 Nilizima TV, Waziri Mkuu Usingizi Ulikata


Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kipigo walichokipata Simba nchini Misri, bado kimemuumiza na kuwaumiza Watanzania wengine.

Simba ilikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Al Ahly katika mchezo wa tatu wa Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Jumamosi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 4, 2019 bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo amewataka Watanzania kuwa wazalendo na timu zao zinapocheza nje ya nchi.

“Asubuhi nilikutana na Mkuchika (Waziri) akawa anaonyesha mkono na kunyoosha vidole vitano, nikakutana na Mwigulu Nchemba naye akawa ananifanyia kama anaendesha bodaboda, nikamuuliza Waziri Mkuu hii maana yake nini, daa ni kipigo cha juzi kweli tulipigwa jamani,” amesema Ndugai na kudai kuwa ilimbid aizime kabisa Tv yake maana hakuweza kuendelea kuangalia.

Spika Ndugai amesema kipigo cha mfululizo kwa timu hiyo kwenye mashindano makubwa ya Ligi ya Mabingwa kinawaumiza wapenzi na mashabiki.

Amewataka wapenzi wa timu nyingine kuunga mkono timu za wenzao wanapocheza na timu za nje ya nchi ili ukifika wakati wote wafanye vizuri.

Hata hivyo aliwatania wabunge kuwa kilichoiponza Simba ni suala zima la baridi ambapo sasa timu ya Al Ahly ikija nchini watalazimika kucheza saa nane mchana ili nao wachezaji wao waumizwe na jua kali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad