Sugu Aachiwa kwa Dhamama Baada ya Sakata la Vitambulisho vya Machinga

Sugu Aachiwa kwa Dhamama Baada ya Sakata la Vitambulisho vya Machinga
MBUNGE wa UJimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jioni hii ambaye alishikiliwa tangu majira ya saa 1 asubuhi ya jana Alhamisi Februari 21, 2019 kwa tuhuma za kutoa/kutumia maneno ya uchochezi akiwa anazungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo.



Sugu anadaiwa kutoa maneno ya kwamba vitambulisho vya wajasiliamali vimetolewa bila elimu na ni sawa na kunawa mikono kisha kwenda kujisaidia.



Kwa mujibu wa RPC Mbeya, Urich Matei ni kwamba Sugu ameonekana katika moja ya clip ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawagi wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogowadogo ‘wamachinga’ na kusema havifai vinastahili kuchomwa moto.



RPC Matei amesema Sugu alisikika akitumia maneno ya kashfa dhidi ya mamlaka iliyotoa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo pia kutumia lugha zinazopinga zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao. Sugu ametakiwa kuripoti tena leo asubuhi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad